MIF na CONAMET Zatia Saini Mkataba wa Ushirikiano Kuimarisha Huduma za Afya na Maendeleo
MIF na CONAMET zimesaini Hati ya Makubaliano (MOU) ya kushirikiana katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo, kwa kuzingatia zaidi sekta ya afya. Ushirikiano huu unalenga kuboresha afya za jamii kwa kutambua kuwa afya bora ni mtaji muhimu wa maendeleo na nyenzo ya kupunguza umasikini.
Kupitia makubaliano haya, taasisi hizi mbili zitafanya kazi pamoja kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya, kuhamasisha kinga na elimu ya afya, pamoja na kusaidia juhudi za kujenga jamii yenye afya, ustawi na uwezo mkubwa wa kushiriki katika shughuli za kiuchumi.